1
قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: لاَ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا, وَلاَ تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا, أَوَلاَ أَدُلُّكُم عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُم, أَفْشُوا السَّلاَمَ بَيْنَكُمْ
Amesema Mtume (s.a.w): ''Hamtaingia peponi mpaka muamini, na hamtakuwa waumini wa kweli mpaka mpendane. Hivi niwafahamishe kitu mkikifanya mtapendana? Salimianeni baina yenu.''
Chanzo: Muslim 1/74.
2
ثَلاَثٌ مَنْ جَمَعَهُنَّ فَقَدْ جَمَعَ الْإِيمَانَ: الْإِنْصَافُ مِنْ نَفْسِكَ, وَبَذْلُ السَّلاَمِ لِلْعَالَمِ, وَالْإِنْفَاقُ مِنَ الإِقْتَارِ
Amesema Ammar bin Yaasir (r.a): 'Mambo matatu anaeyakusanya basi amekusanya Imani, uadilifu wa nafsi yako, na kutoa salamu kwa watu wote, na kutoa (sadaka) hali ya kuwa ni mchache wa mali.'
Chanzo: Al-Bukhari.
3
وَعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: أنَّ رَجُلاً سَأَلَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم أيُّ الْإِسْلاَمِ خَيْرٌ قَالَ: تُطْعِمُ الطَّعَامَ, وَتَقْرأُ السَّلاَمَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ
Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omar (r.a) kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume (s.a.w): 'Ni uislamu gani bora? Mtume (s.a.w) akamjibu: Kulisha chakula (masikini) na kumsalimia unaemjua na usiemjua.''
Chanzo: Al-Bukhari, Muslim 1/65.