1
اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلاَلِكَ عَنْ حَرَامِكَ, وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكِ عَمَّنْ سِوَاكَ
Ewe Mwenyezi Mungui nitosheleze mimi na halali yako kutokana na haramu, na unitosheleze kwa fadhila zako nisiwahitaji wengine wasiokuwa Wewe.
Chanzo: At-Tirmizi 5/560.
2
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْهَمِّ وَالْحَزَنِ, وَالْعَجْزِ وَالْكَسَلِ, وَالْبُخْلِ وَالْجُبْنِ, وَضَلَعِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu, na huzuni, na kutoweza, na uvivu, na ubakhili na uwoga, na uzito wa deni, na kushindwa na watu.
Chanzo: Al-Bukhari 7/158.