Noor
Kiswahili
Noor / Dua / Swala / Adhkari baada ya salamu ya swala

Adhkari baada ya salamu ya swala

Swala · 8 dua

Adhkari baada ya salamu ya swala 0:00
Sikiliza
1

أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ (ثَلاَثَاً) اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلاَمُ, وَمِنْكَ السَّلاَمُ, تَبَارَكْتَ يَا ذَا الْجَلاَلِ وَالْإِكْرَامِ

Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu . (mara tatu). Ewe Mwenyezi Mungu Wewe ndie Amani, na kwako ndiko kunakotoka amani, Umetukuka Ewe mwenyezi utukufu na Ukarimu.

Chanzo: Muslim 1/414.

2

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ, لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ [ثلاثاً], اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ, وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ, وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ

Hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, na yeye ni muweza wa kila kitu, Ewe Mwenyezi Mungu, hapana anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani kwako Wewe ndio (kunakotoka) utajiri.

Chanzo: Al-Bukhari 1/255, Muslim 1/414.

3

لَا إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ, لَهُ الْمُلْكُ, وَلَهُ الْحَمدُ, وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ. لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ, لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ, وَلاَ نَعْبُدُ إِلاَّ إِيَّاهُ, لَهُ النِّعْمَةُ وَلَهُ الْفَضْلُ وَلَهُ الثَّنَاءُ الْحَسَنُ, لَا إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الكَافِرُونَ

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni muweza, hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, wala hamuabudu (yeyote) ila Yeye, ni zake neema, nani wake ubora, na ni zake sifa nzuri zote, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kumtakasia dini yake, japokuwa makafiri wanachukia.

Chanzo: Muslim 1/415.

4

سُبْحَانَ اللَّهِ, وَالْحَمْدُ لِلَّهِ, وَاللَّهُ أَكْبَرُ (ثلاثاً وثلاثين) لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ, لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Ametakasika Mwenyezi Mungu, (mara thelathini na tatu). Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, (mara thelathini na tatu). Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, (mara thelathini na tatu). Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, hali ya kwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, na Yeye ni muweza wa kila kitu. (Kisha atasoma: Suratul-Ikhlas, na Suratul-Falaq, na Suratul-Nnas, (kama inavyojieleza mbele)

Chanzo: Muslim 1/418.

5

بسم الله الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴿قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ* اللَّهُ الصَّمَدُ* لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ* وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُواً أَحَدٌ﴾ بسم الله الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ* مِن شَرِّ مَا خَلَقَ* وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ* وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ* وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ﴾ بسم الله الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ* مَلِكِ النَّاسِ* إِلَهِ النَّاسِ* مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ* الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ* مِنَ الْجِنَّةِ وَ النَّاسِ﴾ (بَعْدَ كُلِّ صَلاَةٍ)

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, Na shari ya alivyo viumba, Na shari ya giza la usiku liingiapo, Na shari ya wanao pulizia mafundoni, Na shari ya hasidi anapo husudu. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, Mfalme wa wanaadamu, Mungu wa wanaadamu, Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, Kutokana na majini na wanaadamu.

Chanzo: Al-Ikhlas:1-4, Al-Falaq:1-5, An-Nas:1-6.

6

اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاءَ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ (عَقِبَ كلِّ صَلاَةٍ)

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.

Chanzo: An-Nasa'i (Hadith no. 100), Ibn As-Sunni (Hadith no. 121,Sahihul-Jami' As-Saghir 5/339, Silsilatul al-Ahadith as-Sahihah 2/697.

7

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ, لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake, hana mshirika wake, ni wake Ufalme na ni zake sifa njema, anahuisha na anafisha, na Yeye ni muweza kwa kila kitu. (mara 10 baada ya swala ya Alfajiri na Magharibi).

Chanzo: At-Tirmizi 5/515, Ahmad 4/227, Zadul-Ma'ad 1/300.

8

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ عِلْماً نافِعاً, وَرِزْقاً طَيِّباً, وَعَمَلاً مُتَقَبَّلاً (بعد السلام من صلاة الفجر)

Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa. (Baada ya kutoa salamu ya swala ya Alfajiri).

Chanzo: Ibn Majah, Sahih Ibn Majah 1/152, Majma' az-Zawaid 10/111.