1
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ
Nakiri kwa moyo na kusema kwa ulimi ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu, peke yake, wala hana mshirika wake, na ninakiri ya kwamba Muhammad (s.a.w) ni mja wake na ni Mtume wake.
Chanzo: Muslim 1/209.
2
اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنَ التَّوَّابِينَ وَاجْعَلْنِي مِنَ الْمُتَطَهِّرِينَ
Ewe Mmwenyezi Mungu nijaalie niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, nijaalie niwe miongoni mwa wale walio safi.
Chanzo: At-Tirmizi 1/78, Al-Albani, Sahih At-Tirmizi 1/18
3
سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ, أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ, أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَيْكَ
Kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zako, nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea kwako. Imepokewa kutoka kwa Aisha (r.a) amesema: Hajapatapo kukaa Mtume (s.a.w) kikao, wala kusoma Qur'an, wala kuswali ila atamaliza na dua hii. Amesema Aisha (r.a) nikamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nakuona hukai kikao chochote wala husomi Qur'an wala huswali swala yoyote ile ila unamalizia kwa kusoma maneno haya, kwanini? Akasema: Ndio anaesema kheri amalize kwa kheri, na anaesema shari yanakuwa maneno haya ni kafara kwake. ''Kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zako, nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea kwako.''
Chanzo: An-Nasa'i, 'Amalul-Yawm wal-Laylah, p. 173, Al-Albani, 'Irwa'ul-Ghalil 1/135, 2/94.