Noor
Kiswahili
Noor / Dua / Asubuhi na Jioni / Kwa anayeona ndoto au njozi ya kutatanisha

Kwa anayeona ndoto au njozi ya kutatanisha

Asubuhi na Jioni · 2 dua

Kwa anayeona ndoto au njozi ya kutatanisha 0:00
Sikiliza
1

يَنْفُثُ عَنْ يَسَارِهِ (ثلاثاً), يَسْتَعِيذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيطَانِ وَمِنْ شَرِّ مَا رَأَى (ثلاث مرات), لاَ يُحَدِّثْ بِهَا أَحَداً, يَتَحَوَّلُ عَنْ جَنْبِهِ الَّذِي كَانَ عَلَيْهِ

Ndoto njema inatoka kwa Mwenyezi Mungu na ndoto mbaya inatoka kwa mashetani. (114) Akiona mmoja wenu ndoto nzuri asimzungumzie ila yule anaempenda, na anaeona ndoto mbaya anatakiwa apulize kushotoni kwake mara tatu. -Kisha atake (aombe) hifadhi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari ya shetani na shari ya alichokiona, mara tatu. -Kisha asilalie ule upande au ubavu aliootea, bali ageukie ubavu mwingine.

Chanzo: Muslim 4/1772, Muslim 4/1773.

2

يَقُومُ يُصَلِّي إِنْ أَرَادَ ذَلِكَ

(115) Atasimama kuswali akitaka.

Chanzo: Muslim 4/1773.