Noor
Kiswahili
Noor / Dua / Swala / Dua ya kufungua swala (Istiftah)

Dua ya kufungua swala (Istiftah)

Swala · 6 dua

Dua ya kufungua swala (Istiftah) 0:00
Sikiliza
1

اللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ, اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ, اللَّهُمَّ اغْسِلْني مِنْ خَطَايَايَ, بِالثَّلْجِ وَالْماءِ وَالْبَرَدِ

Ewe Mwenyezi Mungu niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi, Ewe Mwenyezi Mungu nitakase na madhambi yangu kama vile inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu,Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu.

Chanzo: Al-Bukhari 1/181, Muslim 1/419.

2

سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ, وَتَبارَكَ اسْمُكَ, وَتَعَالَى جَدُّكَ, وَلاَ إِلَهَ غَيْرُكَ

Kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zako, na limetukuka jina lako, na utukufu ni wako, na hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki, asiyekuwa Wewe.

Chanzo: Abu Dawud, Ibn Majah, An-Nasa'i, At-Tirmizi, Al-Albani, Sahih At-Tirmizi 1/77, Sahih Ibn Majah 1/135.

3

وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ حَنِيفَاً وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ, إِنَّ صَلاَتِي, وَنُسُكِي, وَمَحْيَايَ, وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ, لاَ شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ. اللَّهُمَّ أَنْتَ المَلِكُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ, أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ, ظَلَمْتُ نَفْسِي وَاعْتَرَفْتُ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي ذُنُوبي جَمِيعَاً إِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنوبَ إِلاَّ أَنْتَ. وَاهْدِنِي لِأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لاَ يَهْدِي لِأَحْسَنِها إِلاَّ أَنْتَ, وَاصْرِفْ عَنِّي سَيِّئَهَا, لاَ يَصْرِفُ عَنِّي سَيِّئَهَا إِلاَّ أَنْتَ, لَبَّيْكَ وَسَعْدَيْكَ, وَالخَيْرُ كُلُّهُ بِيَدَيْكَ, وَالشَّرُّ لَيْسَ إِلَيْكَ, أَنَا بِكَ وَإِلَيْكَ, تَبارَكْتَ وَتَعَالَيْتَ, أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَيْكَ

Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambae ameumba mbingu na ardhi hali ya kumtakasia yeye dini yangu, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika swala yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa, nami ni katika waislamu, Ewe Mwenyezi Mungu, wewe ndie mfalme, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, wewe ndie Mola wangu na mimi ni mja wako, nimeidhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nisamehe madhambi yangu yote, hakika hakuna mwenye kusamehe madhambi isipokuwa wewe, na niongoze katika tabia njema (nzuri) kwani hakuna mwenye kuongoza katika tabia nzuri isipokuwa wewe, niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wa kuniepusha na tabia mbaya isipokuwa wewe, naitikia wito wako, na shari haitoki kwako, mimi nimepatikana kwa ajili yako, na nitarudi kwako, umetakasika na umetukuka, nakutaka msamaha na ninarejea kwako (kwa kutubia)

Chanzo: Muslim 1/534

4

اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرَائِيلَ, وَمِيْكَائِيلَ, وَإِسْرَافِيلَ, فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ, عَالِمَ الغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقيمٍ

Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa Jibriil na Miikail na Israafil, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliyojificha na yaliyowazi, Wewe unahukumu baina ya waja wako katika mambo ambayo walikuwa wakitofautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale waliyotofautiana kwa ruhusa yako, hakika Wewe unamuongoza umtakae kwenye njia iliyonyooka.

Chanzo: Muslim 1/534

5

اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيرَاً, اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيراً, اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيراً, وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً, وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً, وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً, وَسُبْحَانَ اللَّهِ بُكْرَةً وَأَصِيلاً (ثَلاثاً) أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ: مِنْ نَفْخِهِ, وَنَفْثِهِ, وَهَمْزِهِ

Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mkubwa, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, kwa wingi na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, kwa wingi, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni. (atasema maneno haya mara tatu). Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani, na kupulizia kwake, na kutabana kwake na kutia kwake wasiwasi katika nyoyo za binadamu.

Chanzo: Abu Dawud 1/203, Ibn Majah 1/265, Ahmad 4/85. Muslim 1/420.

6 AI

اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ, أَنْتَ نُورُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ, وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَيِّمُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ, [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّمَواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ] [وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْكُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ] [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِكُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ] [وَلَكَ الْحَمْدُ] [أَنْتَ الْحَقُّ, وَوَعْدُكَ الْحَقُّ, وَقَوْلُكَ الْحَقُّ, وَلِقاؤُكَ الْحَقُّ, وَالْجَنَّةُ حَقٌّ, وَالنَّارُ حَقٌّ, وَالنَّبِيُّونَ حَقٌّ, وَمحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حَقٌّ, وَالسّاعَةُ حَقٌّ] [اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمتُ, وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ, وَبِكَ آمَنْتُ, وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ, وَبِكَ خاصَمْتُ, وَإِلَيْكَ حاكَمْتُ. فَاغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ, وَمَا أَخَّرْتُ, وَمَا أَسْرَرْتُ, وَمَا أَعْلَنْتُ] [أَنْتَ المُقَدِّمُ, وَأَنْتَ المُؤَخِّرُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ] [أَنْتَ إِلَهِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ]

Ee Allah! Sifa njema ni zako; Wewe ni nuru ya mbingu na ardhi na waliomo ndani yake. Sifa njema ni zako; Wewe ndiwe Msimamizi wa mbingu na ardhi na waliomo ndani yake. [Sifa njema ni zako; Wewe ndiwe Mola wa mbingu na ardhi na waliomo ndani yake.] [Sifa njema ni zako; ufalme wa mbingu na ardhi na waliomo ndani yake ni wako.] [Sifa njema ni zako; Wewe ndiwe Mfalme wa mbingu na ardhi.] [Sifa njema ni zako.] [Wewe ni Haki, ahadi yako ni haki, kauli yako ni haki, kukutana nawe ni haki, Pepo ni haki, Moto ni haki, Manabii ni haki, Muhammad (rehema na amani za Allah ziwe juu yake) ni haki, na Kiyama ni haki.] [Ee Allah! Kwako nimesalimu amri, kwako nimetegemea, kwako nimeamini, kwako nimerejea, kwa msaada wako nimehojiana, na kwako nimetaka hukumu. Basi nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyaakhirisha, na niliyoyaficha na niliyoyadhihirisha.] [Wewe ndiwe Mtanguliza na Wewe ndiwe Mwakhirisha; hapana mungu anayestahili kuabudiwa isipokuwa Wewe.] [Wewe ndiwe Mungu wangu; hapana mungu anayestahili kuabudiwa isipokuwa Wewe.]

Chanzo: Al-Bukhari, cf. Al-Asqalani, Fathul-Bari 3/3 , 11/ 116, 13/371, 423, 465. See also Muslim for a shorter account, 1/532.

AI

Maandishi ya Kiarabu na chanzo chake ni sahihi. Vipengele vilivyowekwa alama ya “AI” vimetafsiriwa kimashine katika lugha yako na vinaweza kuwa na makosa — rejeleo ni Kiarabu. Gusa “Ripoti” kwenye kipengele chochote ili kuripoti tatizo.